Peramiho Technologies

Sisi ni kampuni changa ya technolojia bunifu inayojikita katika kuimarisha na kuiboresha jamii kwa kuwezesha mahusiano kati ya wateja na biashara. Bidhaa zetu mbili Peruhu na PeruhuB zimeundwa kurahisisha ugunduzi wa biashara kwa wateja na usimamizi wa biashara kwa wamiliki.

Bidhaa zetu

Peruhu

Peruhu kwa ajiri ya wateja

Peruhu

Programu hii inakusaidia kugundua na kuunganishwa na biashara zinazokuzunguka, kujua huduma zao, maoni na zaidi — yote katika programu moja.

Gundua biashara zinazokuzunguka

Tafuta na ujue biashara kwa urahisi. Pata anwani, maeneo na maelezo ya kina kuhusu huduma, sifa na zaidi katika biashara hizo ili kukusaidia kufanya chaguo sahihi.

Toa maoni yako kuhusu biashara

Shirikisha uzoefu wako kama mteja na soma maoni toka kwa wengine. Hii inakusaidia wewe kufanya maamuzi sahihi na inasaidia biashara kupata mrejesho toka kwa wateja.

  • Piga simu au zungumza na wamiliki wa biashara kwa urahisi ili kupata usaidizi wa haraka.
  • Tafuta biashara kwa urahisi na pata muelekeo wa mahali ilipo biashara hiyo kwenye ramani.
  • Ungana na wateja wengine, tengeneza marafiki na ujenge jumuiya.
  • Peruhu

    Peruhu kwa ajiri ya wamiliki wa biashara

    Peruhu B

    Programu hii inawasaidia wamiliki wa biashara kuunda wasifu wenye nguvu kwa biashara yao na kuwasiliana na wateja ili kuboresha uwepo wao na kujenga uhusiano wa kudumu.

    Gundulika na wateja

    Onesha biashara yako kwa wateja muhimu na ongeza nafasi yako za kugundulika na wale wanaotafuta huduma kama zako. Jitofautishe katika jamii yako na kuvutia wateja zaidi katika eneo lako.

    Pokea maoni muhimu kutoka kwa wateja.

    Jumuika na wateja wako kwa kusoma na kujibu maoni yao. Jenga imani na uaminifu kwa kuonesha unathamini maoni yao na umejizatiti kuimarisha uzoefu wao kama wateja.

  • Pokea simu na kuzungumza na wateja ili kutoa msaada wanaohitaji kwa haraka na kuboresha uzoefu wao kama wateja.
  • Vutia wateja kwa kuonesha huduma zako, orodha ya bidhaa, vyumba, menyu nk.
  • Onesha mazingira ya biashara yako, huduma, eneo na muelekeo.
  • Timu

    Raphael Chaula

    CEO & Founder, Peramiho Technologies

    William Chaula

    COO & Founder, Peramiho Technologies

    Augustino Chaula

    Software Engineer, Peramiho Technologies